Mmenitukania mwanangu hadi tumbo la uzazi limeniuma – Mama Hamisa Mobetto
Mama Mazazi wa Hamisa Mobetto amevunja ukimya kwa kile kinachoendelea kwa sasa.
Mama Hamisa amesema asingependa kuona mwanae anatukanwa mtandaoni kwani ni kitu kinachomuumiza sana. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
Mmenitukania Mwanangu hadi Tumbo la Uzazi limeniuma , natamani ningewazaa wawili ili ajifariji kwa mwenzie.Pia ningeomba familia zote zilizopo Instagram, Mpunguzieni matusi na kumdharilisha Mwanangu, kama kawakosea ninamwombea Msamaha mwezi huu mtukufu . .Mpeni Amani ili na mimi nifurahie furaha ya Uzazi wangu. Ni mwenyezi Mungu pekee huchagua barabara atakayopitia Mwanaadamu.
Comments
Post a Comment